30 Aprili 2015 - 18:49
Iran yatuma meli za kivita Yemen

Meli mbili za kivita za Iran zimewasili katika mlango bahari wa Bab el-Mandab , ambapo ni njia muhimu ya maji baina ya Yemen na Djibouti.

Meli  mbili za  kivita  za  Iran zimewasili  katika  mlango bahari  wa Bab el-Mandab , ambapo ni njia muhimu ya  maji  baina ya  Yemen  na Djibouti. 

Katika  ishara  nyingine  inayoleta  wasi  wasi   baina  ya  nchi mahasimu  katika  eneo  la  ghuba  Iran  na  Saudi  Arabia , afisa  wa ubalozi  wa Saudi Arabia anayehusika  na  masuala  ya  kijeshi ametakiwa  kufika  katika  wizara  ya  mambo  ya  kigeni mjini Tehran  kusikiliza malalamiko  makali  kuhusiana  na  hatua  za kijeshi  za  Saudi  Arabia  ambazo  zimezuia  ndege  ya misaada kutoka Iran  kutua mjini  Sanaa.

Mkuu  wa  jeshi  la  majini  la  Iran  admirali Habibollah Sayari amenukuliwa  na  shirika  la  habari  la  Iran IRNA  akisema  meli hizo  ziko  katika  ghuba  ya  Aden  kwa  mujibu  wa  sheria  za kimataifa  kuhakikisha  usalama  wa  meli  za  kibiashara  za  nchi hiyo dhidi  ya  kitisho cha  uharamia.